CRDB Bank kupitia Tawi lake la Kilwa imekabidhi seti moja ya jezi kwa Timu ya Mpira wa Miguu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza ushirikiano kati ya taasisi hiyo ya kifedha na serikali.
Makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 19 Agosti 2025, ambapo jezi hizo zimekabidhiwa na Meneja wa CRDB Tawi la Tanga Jiji kwa niaba ya benki hiyo.
Jezi hizo zinatarajiwa kutumika katika mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea jijini Tanga, ambapo timu hiyo inawakilisha Halmashauri ya Kilwa.
Uongozi wa Halmashauri umeipongeza CRDB kwa mchango wake, unaoonesha dhamira ya kweli ya benki hiyo katika kuunga mkono shughuli za kijamii, hasa kupitia michezo inayochochea mshikamano, afya na motisha kazini.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa