Watanzania wametakiwa kuendelea kuheshimu na kutunza utamaduni ambao ndio urithi ambao unalifanya Taifa liendelee kuwa hai.
Wito huo umetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipotembelea shughuli za tamasha la utamadini wa Mtanzania ,jamii ya watu wa Lindi hilo linalofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam Oktoba 26, mwaka huu.
Majaliwa amesema suala la kuuenzi utamaduni ni jambo zuri ambalo linatoa fursa kwa watu wengine hususani wa mataifa ya nje kuja kujifunza historia ya Watanzania na maisha yao.
“Nimefurahi kuona nyumba zikiwa na zana mbalimbali za kitamaduni ambazo zilikuwa zikitumiwa na wazee wetu pamoja na namba ya utayarishaji wa vyakula vyetu vya asili
“Sikutarajia kuona haya ninayoyaona, nawashukuru wote walioshiriki katika kandaa tamasha hili pamoja na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Kijiji cha Makumbusho.” Alisema Majaliwa.
Waziri Mkuu alisema tamasha hilo ambalo limewakutanisha Wanalindi kutoka katika wilaya mbalimbali linatoa fursa ya wao kujadili maendeleo ya mkoa wao na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Majaliwa amewaomba wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda katika Kijiji cha Makumbusho kwa ajili ya kujifunza historia ya mkoa wa Lindi pamoja na fursa zilizopo.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema mkoa umetumia tamasha hilo kutoa ujumbe kwa umma kuhusu vivutio mbalimbali walivyonavyo pamoja na fursa za uwekezaji.
Chanzo - www.ruangwadc.go.tz
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa