Kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo kimeanzisha kampeni ya kufanya mazoezi ya pamoja ya viungo kila siku ya Jumamosi, kwa lengo la kuhamasisha jamii kuzingatia umuhimu wa afya bora ya mwili na akili.
Katika Jumamosi ya leo Tarehe 03/05/2025,wananchi wa Kata ya Masoko wamejumuika kwa mazoezi ya pamoja yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa/Mwenge. Mazoezi hayo yalishirikisha makundi mbalimbali wakiwemo Walimu na Wanafunzi kutoka Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi, Watumishi wa Halmashauri, pamoja na Wafanyakazi kutoka Benki ya NMB.
Afisa Utamaduni,Sanaa na Michezo Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bi.Veneranda Maro akishiriki katika Mazoezi hayo amesema:
“Mazoezi haya si tu kwa ajili ya afya ya mwili, bali pia yanasaidia kuunganisha jamii na kupunguza msongo wa mawazo.”
Aidha, mmoja wa washiriki wa mazoezi hayo, Bw. Juma Ally, alisema: “Ni jambo jema na la kuigwa. Tunaomba yafanyike mara nyingi zaidi ili vijana na wazee wote wawe na nafasi ya kushiriki.”
Mazoezi haya ni endelevu na yanatarajiwa kufanyika kila Jumamosi. Wananchi wote wanahimizwa kujitokeza kwa wingi ili kushiriki na kujenga afya bora kwa pamoja.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa