Mwezeshaji wa mafunzo ya Elimu ya Awali kutoka Ofisi ya Rais, (TAMISEMI) Ndg,Verena David Nchimbi, amewataka Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Awali Wilayani Kilwa kuimarisha umahiri na ubunifu katika ufundishaji wa Watoto wa elimu ya awali.
Ndg. Verena ameyasema hayo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku nne kwa walimu wapatao 140 kutoka shule za msingi 70 Wilayani humo, yatakayofanyika kuanzia tarehe 19/12/2024 mpaka 22/12/2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kilwa.
Aidha Ndg. Verena amewata walimu kuondoa fikra potofu iliyopo kwa wazazi kuwa, watoto wa elimu ya awali wanapoteza muda mwingi wakicheza shuleni, Hivyo walimu watoe elimu kwa wazazi juu ya mitaala na hatua zinazofuatwa katika ufundishaji wa watoto hao.
“Kuimba na kucheza ni mbinu mojawapo ya mwalimu kumuwezesha mtoto kusoma na kuandika, Nawasihi waalimu muipinge kauli ya kusema mtoto anaenda kucheza shuleni, inapobidi muwaonyeshe namna watoto wao wanavyoelewa kupitia michezo’’ amesema Ndg. Verena
Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Msingi Ndg. Mshamu Ndandavale kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, ameshukuru Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kwa kuandaa mafunzo hayo yatakayoleta tija na kuinua sekta ya elimu wilayani Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa