Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi amewataka wakuu wa Wilaya zinazounda Mkoa huo kuunda Kamati za kutatua na kushughulikia migogoro ya wafugaji na wakulima katika Wilaya zao.
Zambi ametoa agizo hilo katika kijiji cha Nangurukuru Wilaya ya Kilwa alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta ya mifugo waliopo mkoani humo ikiwa ni mkakati wa kumaliza migogoro baina ya wakulima na wafugaji.
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wakuu hao wa wilaya kuunda kamati za kudumu zitakazo wajumuisha wataalamu wa halmashauri, vyombo vya ulinzi na usalama na wakuu wa wilaya ambao wataratibu na kusimamia utendaji wake ambazo zitakuwa zinashugulikia na kutatua migogoro na wakulima.Huku akizitaka kamati zitakazo undwa kumpelekea taarifa kila baada ya miezi mitatu.
Zambi amezitaka kamati hizo kumpelekea taarifa kila baada ya miezi mitatu,alisema amelazimika kutoa agizo hilo ili kila wilaya ishugulikie na kutatua migogoro na changamoto nyingine baina ya makundi hayo mawili ya kijamii.Huku akiweka wazi kwamba hatarajii kusiikia tena migogoro.Kwani kila itakapotokea itashugulikiwa haraka.
Alisema kamati hizo zishirikiane kwa karibu na viongozi wa serikali za vijiji ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi zitakozowezesha kushughulikia kikamilifu migogoro na changamoto nyingine ili mkoa uendelee kuwa na amani na utulivu.
Katika kuhakikisha kamati hizo hazikwami katika utendaji wake,amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kuziwezesha usafiri ili ziweze kufika katika maeneo ambayo zitakiwa kwenda nakutekeleza majukumu yake.Lakini pia uwezeshaji huo usingize na malipo ya posho.Bali usafiri,hasa mafuta.
Amezitaka zihakikishe wakulima wanalima kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo.Hali kadhalika wafugaji wafugie kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ufugaji.Akiitaka pia ihakikishe wakulima hawazuii na kuziba njia zinazotumiwa na wafugaji kwenda kunywesha mifugo yao mitoni.
Aidha mkuu huyo wa mkoa ameziagiza halmashauri zote zihakikishe zinasimamia na kutekeleza kikamilifu mpango wa matumizi bora ya ardhi katika kila kijiji.Hata kama halmashauri nyingine hazina wafugaji.Kwani lengo nikila kijiji kiwe kimefanya mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Katika hali iliyoonesha mkuu huyo wa mkoa ameamua kumaliza kabisa migogoro mkoani humu.Amewaonya vingozi na watendaji wa vijiji kwamba yeyote atayebainika kuingiza mifugo kinyemela(Bila kufuata sheria),atapoteza kazi na kuondolewa kwenye uongozi.
"Upo mtindo wa wafugaji kuwafuta wenzao,waambie wenzenu(wafugaji) wanaotaka kuja huku wasije kwanza hadi tuhakiki idadi ya mifugo iliyopo na mahitaji halisi.Mfugaji atayeingiza mifugo kinyemela atarudishwa alikotoka.Viongozi na watendaji wa vijiji watakao bainika walishiriki mchezo huo tutawaondoa madarakani," alisisitiza Zambi.
Katika kukabiliana na changamoto ya miundombinu,Zambi alitoa wito kwa wafugaji kusaidiana na serikali kujenga msjosho na maranbo.Kwani miongoni mwa mambo yanayosababisha migogoro ni tatizo la maji.Hasa kipindi cha kiangazi.
Kikao hicho kilichowashirikisha wakuu wawilaya,maofisa mifugo,wanyeviti na wakurugenzi wa halmashauri,maofisa ardhi,wafugaji na wakulima na wataalamu na maofisa wa ofisi ya mkuu wa mkoa kilimalizika na kutoa maazimio 14 ambayo yanatakiwabkufanyiwa kazi.
Miongoni mwa maazimio hayo ni wafugaji waanzishe uongozi kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa,kuanzishwa ushirika wa wafugaji,mkoa kuwa na vituo vya ukaguzi wa mifugo inayoingia mkoani humu,halmashauri kujenga machinjio ya kisasa na minada na kuboresha iliyopo.
Mkoa wa Lindi nimiongoni mwa mikoa iliyppokea wafugaji kutoka mkoa wa Mbeya mwaka 2006.Hadi sasa niwilaya halmashauri za Ruangawa na manispaa ya Lindi pekee ndizo hazijapokea wafugaji.Hata hivyo kumekuwa kukitokea migogro michache na midogo baina ya wakulima na wmafugaji.Hasa miaka ya mwanzo wakati wafugaji wanaingia mkoani humu.
Chanzo:Muungwana Blogu
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa