Wadau mbalimbali na watumishi kutoka Taasisi na Sekta mbalinbali wamiminika kutembela banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 ndani ya viwanja vya Chinangali Dodoma.
Banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi linalojuimuisha halmashauri zake zote sita zimeshiriki maadhimisho hayo kwa namna ya kipekee ambapo zimekuja na mifumo rafiki ya kutoa huduma kwa wananchi kwa njia raisi kama vile mfumo jumuishi wa kutoa huduma kwa wananchi (One Stop Centre ), Kadi-Alama, fursa za uwekezaji Mkoa wa Lindi, mfumo wa kidigitali wa usimamizi rasilimali watu wa ndani na mfumo wa hewa ukaa unaotekelezwa halmashauri ya Mtama.
Hayo ni baadhi ya mambo yanayowavutia wengi kuja kujifunza katika banda la Mkoa wa Lindi
Karibu sana katika Banda la Mkoa wa Lindi ili kuzijua fursa mbalimbali zinapatikana Lindi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa