Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilayani Kilwa Ndg. Shija Lyella amewataka wafugaji wilayani Kilwa kutengeneza uhusiano mzuri na jamii wanazoishi nazo ili kuzuia kutokea kwa migogoro wakati wa uanzishaji wa vitalu vya malisho ili kuweza kufikia dhima ya uanzishaji wa vitalu hivyo.
Ameyaeleza hayo leo tarehe 05/03/2025 katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa wakati wa kikao baina Wataalamu kutoka Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Chama cha Wafugaji na Viongozi wa wafugaji wa kutoka kila kata, ambapo wamejadili juu ya mpango wa kuanzisha vitalu vya malisho vitakavyosaidia katika shughuli za ufugaji na kupunguza migogoro ya ardhi inayojitokeza katika jamii.
Akitoa elimu kuhusiana na matumizi na utunzaji wa vitalu hivyo Afisa Mifugo Ndg. Stanford Mwamlima amesema kuwa mbali na faida ya kuondoa migogoro ya ardhi kupitia ugawaji wa vitalu pia mpango huo utasaidia wafugaji kumiliki ardhi zao na kupunguza changamoto ya kuhamahama, kuimarisha mahusiano mazuri baina ya wafugaji na wamiliki weingine wa ardhi na uboreshaji wa masoko ya mifugo kwa wafugaji hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Kanda ya Kusini Ndg. Rashidi Kalele kwa niaba ya wafugaji ameipongeza Halmashauri kwa hatua hiyo ambayo itaenda kusaidia kuondoa migorogoro ya ardhi katika jamii. Pia amewataka wajumbe wa kikao hicho kwenda kuwaeleza wananchi juu ya umuhimu wa mpango huo.
Ikumbukwe Zoezi hili linafuata baada ya Halmashauri ya Wilaya ya kilwa kuandaa wataalamu waliopatiwa mafunzo katika Wilaya ya Kibiti juu ya uendeshaji wa ranchi za mifugo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa