Wananchi wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kutumia dhana ya utamaduni ili kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Habari, Sanaa, utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe alipokuwa akifungua Tamasha la utamaduni la Watu wa Mkoa wa Lindi linalofanyika katika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam Oktoba 25 mwaka huu.
Mheshimiwa Mwakyembe amesisitiza wananchi wa Lindi kujishughulisha na masuala ya utamaduni kama vile kuhifadhi na kutunza maeneo ya kihistoria yatakayowavutia watalii kutoka maeneo mbalimbali.
“Kwa kupitia utamaduni mtaweza kujikwamua kiuchumi amueni kufanya utamaduni kuwa ni chanzo cha kuleta maendeleo, pia nawapongeza kwa nia ya dhati kabisa na ninawasaa jamii nyingine kuinga mfano wa wanalindi katika kuenzi utamaduni” alisema Mwakyembe
Mwakyembe amesema kuwa Wizara ya Habari,Sanaa,utamaduni na Michezo itaendelea kuunga mkono wadau wanaoshughulika na kazi ya kulinda na kutunza utamaduni wa taifa na kusema kuwa taifa bila utamaduni ni sawa na taifa mfu.
“Suala la kutunza na kuendeleza utamaduni si suala la Serikali tu ni wajibu wajibu wa kila mwananchi kufanya hivyo hivyo tusaidiane kuendeleza na kukuza tamaduni zetu” alisisistiza Mwakyembe.
Aidha Waziri Mwakyembe amepongeza uongozi wa Mkoa wa Lindi kwa dhamira njema ya kufanya tamasha la utamaduni na kuendeleza michezo. Pia Waziri Mwakyembe ameipongeza Wilaya ya Ruangwa kwa kujenga Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Majaliwa Stadium uliopo Wilayani humo.
Tamasha la utamaduni wa Mtanzania mwaka 2018 limeshirikisha Jamii za Watu wa Mkoa wa Lindi ambapo kila Wilaya inayounda Mkoa wa Lindi inaonyesha Mila na Desturi zake.
Tamasha la utamaduni la Mkoa wa Lindi Linafanyika kwa siku nne kuanzia Oktoba 25 hadi Oktoba 28 katika Viunga vya Kijiji cha Makumbusho , Kijitonyama Jijini Dar es salaam huku kauli mbiu yake ikiwa ni "Lindi utamaduni wetu, Urithi wetu kwa maendeleo".
Chanzo - www.ruangwadc.go.tz
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa