Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi leo tarehe 26 Januari, 2025 imetoa Elimu ya Mpiga Kura kwa kutumia Gari la Elimu ya Mpiga Kura katika kata za Masoko, Kivinje, Tingi na Somanga zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
Lengo ni kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika kata zao litakalodumu kwa muda wa siku saba (7) kuanzia tarehe 28 January hadi 03 Februari, 2025.
Lengo la uboreshaji wa daftrai la kudumu la wapiga kura ni kuandikisha wapiga kura wapya ambao tayari wana miaka 18, au wale watakokuwa na miaka 18 kabla au ifikapo siku ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kuhamisha taarifa za watu waliohama makazi, kurekebisha taarifa zilizokosewa, kutoa kadi mpya kwa watu waliopoteza kadi au kuharibika, Lakini pia kuondoa taarifa za watu waliopoteza sifa za kupiga kura.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa