Afisa Forodha Mfawidhi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Lindi Bi. Flora Kijole na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Yususph Mwinyi, wamefanya makabithiano rasmi ya mzigo wa sukari ya magendo wenye thamani ya TSh. 6,100,000/=
Mzigo huo ulipatikana ukiingizwa nchini kinyume cha sheria katika operesheni maalumu ya kuthibiti magendo iliyotekelezwa na Maafisa Wa Forodha Mkoa wa Lindi kwa kushirikiana na Vyombo vya ulinzi na Usalama, pembezoni mwa bahari wilayani Kilwa. Makabithiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tarehe 25 Oktoba 2024.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa