Kilwa,
Timu ya soka Halmashuri ya wilaya ya kilwa imekubali kipigo cha goli 2 bila majibu kutoka kwa timu ya soka ya Halmashauri ya Wilaya Mtwara wana Kuchele.
Mchezo huo wa kirafiki umepigwa katika Uwanja wa Mwenge (Taifa) Mjini Kilwa Masoko ukiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Halmashauri ya Wialaya ya Kilwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Sanjari na mchezo wa Soka michezo Kadhaa ilichezwa katika kusindikiza Bonanza hilo ambapo Timu za Mpira wa Pete na Wavu za Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa zilkubali kipigo kutoka kwa Halmashauri ya Mtwara huku kilwa ikibuka kidedea katika mchezo wa Drafti na Bao.
Timu ya soka ya maveterani kutoka kilwa Masoko ilitoka suruhu dhidi ya Jeshi la polisi katika mechi ya ufunguzi iliyopigwa mapema katika uwanja wa Mwenge (Taifa).
Akifunga mashindano hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa , Katibu tawala wa Wilaya ya Kilwa Ndg. Haji Balozi ameipongeza Halmashauri ya Mtwara kwa ushindi na kuwashukuru kwa ushiriki wao katika Bonanza hilo.
Aidha ameshauri kuwepo kwa zawadi kwa washindi katika Bonanza lingine katika siku za usoni.
Sanjari na Michezo mbalimbali pia kulikuwa na zoezi la uchangiaji Damu salama ambapo jumla ya Chupa 5 za damu zilipatikana.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa