Taasisi ya Uhifadhi na Maeneo Tengefu Tanzania (MPR) chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa matumbawe kwa ajili ya kukuza ustawi wa sekta ya uvuvi wilayani Kilwa.
Akifungua mafunzo hayo tarehe 8 Oktoba 2025 katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Nyundo, amesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika shughuli za uhifadhi ili waweze kuelewa faida na fursa zinazotokana na hifadhi ya matumbawe.
Mafunzo hayo yameambatana na mrejesho wa taarifa kuhusu uandaaji wa miundombinu ya uhifadhi nchini, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha usimamizi endelevu wa rasilimali za bahari.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Afisa Uvuvi Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Upendo Hamidu ameeleza umuhimu wa kuanzishwa kwa maeneo ya hifadhi ya bahari, ikiwemo kuchochea ukuaji wa shughuli za utalii na kuongeza kipato cha wananchi.
Nae Mwezeshaji Ndg. Godfrey W. Ngupula amesema uhifadhi huo utasaidia kukuza uvuvi wa kitaalamu na kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu vinavyohatarisha mazingira ya baharini.
Akiongeza, amesema taasisi hiyo itaendelea kuhakikisha ushirikishwaji wa wananchi katika hatua zote za uhifadhi, ikiwemo upangaji, utekelezaji na ufuatiliaji wa shughuli za hifadhi, ili kujenga umiliki wa pamoja katika kulinda rasilimali za bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Nyundo, ameipongeza Marine Park and Reserve Unit kwa juhudi zake za kuelimisha jamii na kusimamia uhifadhi wa rasilimali za bahari, akibainisha mchango wake mkubwa katika kukuza uchumi wa bahari.
Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Taasisi ya Uhifadhi na Maeneo Tengefu kwa kutoa elimu hiyo muhimu, wakibainisha kuwa itawasaidia kuongeza uelewa na kuchukua hatua za pamoja katika kulinda rasilimali za bahari kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa