Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imetenga kiasi cha shilingi milioni 130 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa ya kidato kwanza 2020.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ndg Renatus Mchau alipokutana na watendaji wa kata zenye shule za sekondari zenye uhaba wa vyumba vya madarasa 2020.Akitoa taarifa hiyo ,ndg Mchau alieza kuwa Ofisi yake imepokea taarifa inayoonesha uwepo wa upungufu wa madarasa 20 katika shule 11 kati ya shule 26 za Wilaya ya Kilwa.
Mkurugenzi alitoa taarifa kuwa kwa kuanza ofisi yake imetenga jumla ya shilingi milioni 130 ambapo mgawanyo wake ni shilingi milioni sita na laki saba (6,700,000) kwa kila darasa katika shule hizo 11.
Akitoa mchanganuo wa shule zenye upungufu wa madarasa, Kaimu Afisa Elimu Sekondari Mwl.Bujiku Sakila alizitaja shule zenye upungufu wa chumba kimoja kila shule kuwa ni ;Alli Mchumo,Kibata, Nakiu na Kikanda, Pia alieleza kuwa shule zenye upungufu wa madarasa mawili kila moja ni; Kipatimu, Kiranjeranje,Kivinje, Mpunyule na Mingumbi huku shule ya sekondari ya Mtanga iliopo kata ya Masoko ikiwa na upungufu wa madarasa matatu.
Katika kikao hicho ,watendaji wa kata zenye uhaba wa madarasa walieleza hatua mbali mbali walizotumia katika kukabiliana na upungufu huo ambapo baadhi ya watendaji walikuwa kwenye hatua ya upauaji wa majengo huku wengine wakisubiri msimu wa mvua kupungua ili kuweza kuweza kuanza ujenzi kutokana na mapato ya ndani ya kata zao na michango toka kwa wananchi na wadau wa maendeleo katika maeneo yao.
Upungufu huu umetokana na ufaulu wa asilimia 72 ya wanafunzi wote waliomaliza darasa la saba mwaka 2019 ambapo jumla ya wanafunzi 3065 walifaulu kujiunga na elimu ya sekondari 2020 kati yao wanafunzi 963 walikosa nafasi kutokana na upungufu wa vyumba vya maradarasa.
Mwl.Bujiku alieleza kuwa kwa mwaka 2019 wanafunzi waliomaliza kidato cha nne ni wanafunzi 1240 hali iliyopelekea kutokuwa na uwiano sawa kati ya idadi ya wanafunzi wanaomaliza na wanatakiwa kujiunga kidato cha kwanza 2020.
Mkurugenzi aliwataka watendaji na waratibu elimu kata kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi atakayekosa shule kwa visingizio vya ukosefu wa madarasa katika kata zao pia aliwasisitiza kuzingatia sharia za ununuzi na ujenzi ili kuwezesha kupatikana majengo bora.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa