Kilwa,
Halmashauri ya wilaya ya kilwa imegawa miche 20954 ya mikorosho kwa wananchi wilayani hapo ikiwa ni jitihada za kukuza zao la korosho pamoja na kuongeza pato kwa wakulima na halmashauri kupitia zao la hilo.
Uzinduzi wa ugawaji na upandaji wa miche hio umefanyika Januari 19 katika vitaru vya halmashauri ya wilaya ya kilwa vilivyopo eneo la mtanga, hafla ambayo iliudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya kilwa ikiongozwa na mwenyekiti wake mkuu wa wilaya ya kilwa Mh. Christopher Ngubiagai , mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya kilwa, wakuu wa idara mbalimbali na wananchi kutoka sehemu mbalimbali za viunga vya wilaya ya kilwa.
Mkurugenzi wa halmashauri wilaya ya Kilwa Bw. Zablon Bugingo (katikati) akisisitiza jambo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ugawaji miche ya mikorosho uliofanyika januari 19, katika vitaru vilivyopo eneo la mtanga, wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya kilwa Mh. Christopher Ngubiagai.
Akizungumza baada ya hafla hio Afisa kilimo wilaya ya Kilwa Bw. Mkinga amewashukuru wananchi waliojitokeza kuchukua miche ya mikorosho kwa kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza zao hilo pamoja na kukuza pato la wakulima na taifa kwa ujumla.
Aidha, Mkinga amewataka wakulima kufuata maelekezo waliyopewa ya jinsi ya kupanda na kuhudumia miche hio na kuahidi kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kuangalia maendeleo ya miche hio.
miche ya mikorosho ilioteshwa na halmashauri ya wilaya ya kilwa
halmashauri ya wilaya ya Kilwa kwa kushirikiana na wataalamu kutoka idara ya kilimo imeotesha miche milioni moja ya mikorosho ambayo inagawiwa bure kwa wakulima.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa