Watu wanne wamekamatwa katika bahari ya Hindi wilayani Kilwa mkoani Lindi kwakukutwa wakivua jongoo wa bahari na kamba kochi kwa kutumia Dhana haramu za uvuvi.
Akieleza tukio hilo ofisa uvuvi wa wilaya ya Kilwa,Kengela Mashimba .Alisema watu hao walikamtwa juzi saa nane mchana karibu na kisiwa cha Simaya,kilichopo katika bahari ya Hindi.
Mashimba alisema watu hao ambao wawili kati yao hawakuwa na leseni ya uvuvi walikutwa na mashine iliyokuwa inawapa hewa ya oksijeni nakuwafanya wamudu kukaa chini ya maji kwa takribani saa sita huku wakikusanya jongoo na kamba kochi wakubwa na wadogo.Kwani walikuwa wanatumia nyavu zenye matundu madogo ambazo zimekazwa kisheria kutumika kuvulia.
Alisema watu hao ambao walikutwa wakiendelea kukusanya jongoo na kamba kochi wadogo ambao nimiongoni mwa rasimali za baharini ambazo zimekatazwa kuvuliwa.Akiweka wazi kwamba kitendo hicho kimezuiwa na sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 ambayo kanuni zake zilianza kutumika mwaka 2009.
"Tuliwakuta na Saratoga (compressor) ambayo ilikuwa inawapatia hewa wakiwa baharini.Jongoo bahari hawana kasi ya kutembea.Kwahiyo walikuwa wanauwezo wakusanya kirahisi.Lakini wawili kati yao hawakuwa na leseni za uvivu.Kibaya zaidi walikuwa wanatumia nyavu zenye matundu madogo ili wazoe kila saizi,"alisema Mashimba.
Ofisa uvuvi huyo ambaye hakutaka kuweka wazi majina ya waliokamatwa wala chombo cha usafiri na namba zake za usajili alisema licha ya watu hao wanne,lakini pia mmiliki wa chombo kilichokuwa kinatumiwa na wavuvi hao haramu amekamatwa.
"Siwezi kutaja majina wala namba za usajili wa chombo hicho kwasababu tukio limetokea juzi inawezekana wameshafikishwa mahakamani.Kwahiyo sipendi kuingilia mwenendo wa kesi iliyopo mahakamani," alisema kwa tahadhari.
Mashimba alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na vikundi vya ulinzi shirikishi vya ulinzi wa rasilimali za baharini na pwani(BMU)na maofisa wa idara ya uvuvi.Kwani hata kukamatwa kwa watu hao kulifanywa na maofisa wa idara ya uvuvi na walinzi hao baada ya kupata taarifa kwa raia wema.
Akitoa maoni yake kuhusu tukio hilo,mkuu wa wilaya ya Kilwa,ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya hiyo,Christopher Ngubiagai licha ya kuwapongeza maofisa uvuvi na walinzi shirikishi hao.Alisema doria na misako dhidi ya wavuvi wasiozingatia sheria ni endelevu.Huku akitoa wito kwa wavuvi kuanza kufikiria kufuga samaki badala ya kung'ang'ania kuvua baharini kwakutumia zana haramu za kuvulia.
Ngubiagai alitoa wito kwa wanasiasa waliopo wilayani humo washiriki kikamilifu katika mapambano yakukomesha uvuvi haramu.Huku akiweka wazi kwamba baadhi yao ni kikwazo katika mapambano hayo.
Kwamujibu wa mkuu huyo wa wilaya misako na doria hizo zimesababisha uvuvi haramu kupungua na upatikanaji wa samaki unaongezeka kwa kasi wilauani humo.
NEWS CREDIT: MUUNGWANA BLOG
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa