Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kupitia Idara ya Afya na kitengo cha Tehama imeendesha Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa GoT-HOMIS Centralized kwa Waganga Wafawidhi na Wafamasia wa Vituo vya Afya pamoja na Zahanati (55) lengo ikiwa ni kuboresha utunzaji wa Taarifa za wagonjwa na ukusanyaji wa Mapato kwenye Vituo vya Afya na Zahanati.
Aidha Mafunzo hayo yamelenga kuongeza Ubora na Ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa kwenye vituo vyao vya kazi.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa Siku Nne kuanzia Januari 13 hadi 16, 2025 katika Ukumbi wa Chuo Cha Maendeleo (FDC)Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa