Kilwa,
Madiwani wilayani kilwa wametakiwa kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato na kuibua vyanzo vipya vya mapato katika kata zao.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Mhe. Swahaba Matajiri alipokua akiwasilisha mapendekezo ya kamati ya huduma za jamii katika kikao maalum cha baraza la madiwani kilicho kaa kupitia na kujadili mipango na bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya kilwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika februari 21 katika ukumbi wa jumba la maendeleo mjini kilwa masoko.
Mhe. Matajiri amesema iwapo madiwani watasimamia ukusanyaji wa mapato vilivyo tatizo la ufinyu wa bajeti katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo litakua limepatiwa ufumbuzi.
Aidha amewataka madiwani kubuni vyanzo vingine vya mapato katika kata zao ili kuongeza pato ambalo litasaidia kutatua kero mbalimbali ambazo zinazikabili kata hizo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya kilwa Bw. Kaunda amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanatumia vizuri fedha zinazotolewa na halmashauri kwa ajili ya kukamilisha miradi na zitumike katika miradi husika.
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 halmashauri imepanga kukusanya na kutumia jumla ya Bilioni arobaini na nne, milioni mia tisa ishirini na saba, laki tisa thelethini elfu mia moja tisini na tatu (44,927,930,193.00) ili kuweza kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa