Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wameagwa kwa heshima kubwa na viongozi pamoja watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ambapo hafla hiyo imefanyika tarehe 19 Juni 2025 katika viwanja vya nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Nyundo amewapongeza madiwani kwa utumishi wao uliotukuka na mchango wao katika maendeleo ya wilaya, pia amewataka kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo hata baada ya kumaliza muda wao wa uongozi.
Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilwa Ndg. Yusuf Mwinyi amewapongeza madiwani hao kwa jitihada zao katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika miaka 5 ambayo imepelekea Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kupata hati safi kutoka kwa Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa hesabu za serikali CAG.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Hemed S. Magaro amewashukuru madiwani kwa ushirikiano wao na kusema kuwa mafanikio yaliyopatikana yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mshikamano kati ya madiwani na watendaji wa halmashauri.
Kwa niaba ya madiwani wote, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Farida Kikoleka, amewashukuru viongozi wa Wilaya na watumishi wa halmashauri kwa ushirikiano waliowapa kipindi chote cha uongozi wao, pia amewataka waendelee kushirikiana nao hata katika shughuli nyingine za kijamii na kimaisha.
Hafla hiyo imehitimishwa kwa chakula cha pamoja na utoaji wa vyeti vya kutambua mchango wa madiwani hao kwa maendeleo ya Wilaya ya Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa