Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Ndg. Hemed S. Magaro amewapokea madaktari bingwa na bingwa bobezi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kutoa huduma za afya wilayani humo.
Huduma zitakazotolewa zitahusisha magonjwa ya wanawake na ukunga, watoto na watoto wachanga, upasuaji, usingizi na ganzi, magonjwa ya ndani(Kisukari, Shinikizo la damu n.k) pamoja na magonjwa ya kinywa na meno.
Huduma hizo zitatolewa katika Hospitali za Wilaya Kinyonga na Kipatimu kuanzia tarehe 15 hadi 19 Septemba 2025.
Wananchi wote Mnakaribishwa!
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa