Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed S. Magaro amefungua Mafunzo ya muda wa siku mbili (2) kuanzia tarehe 21-22/01/2025, kwa Maafisa Waandikishaji Wasaidizi Ngazi ya Kata Kwa majimbo Mawili (Kilwa Kusini na Kilwa Kaskazini) ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
Lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Maafisa Waandikishaji Ngazi ya Kata, kwa ajili ya kuboresha Daftari la kudumu la Wapiga Kura. Katika Mafunzo hayo Maafisa watafundishwa namna ya ujazaji fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura, (Voters Registration System- VRS).
Akifungua mafunzo hayo Ngd. Magaro amewataka washiriki wa mafunzo kusikiliza kwa makini kwa kuwa mafunzo hayo yanawajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao, Pia amewataka kutunza vifaa, kushirikiana na maafisa Ngazi ya Jimbo na kuhamasisha wananchi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kujiandaa na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2025.
Aidha, Ndugu Magaro ameeleza kwamba Mawakala wa Vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura, ili kuleta uwazi katika zoezi zima na kuwatambua waombaji katika maeneo yao, hata hivyo mawakala hao hawataruhusiwa kuingilia utekelezaji wa majukumu ya Watendaji.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa