Katika kuendeleza mapambano ya kupinga Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kupitia kitengo cha Ustawi wa Jamii imeendeleza shughuli za kupambana na Ukatili wa Kijinsia ikiwemo; kupokea Mashauri 65 ya ukatili kwa Watoto ambapo kati ya hayo kesi tano (5) zimefikishwa Mahakamani, Pia Wanawake 237 wamepatiwa huduma dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.
Aidha Kitengo kimefanikiwa kutoa huduma za Ustawi wa Jamii katika Vituo vya Afya 20, Kutoa msaada wa Kisheria Kupitia Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) katika Kata 10 na Vijiji 30, Kutoa Elimu kwa watu 7,735 Kuhusu Haki za Watoto, Ndoa, Ardhi, Ajira na Ukatili wa Kijinsia.
Hayo yamezunguzwa na Afisa Ustawai wa Jamii Wilaya ya Kilwa Bi. Charity Ngenzi katika kikao cha Kujadili taarifa za Utekelezaji wa Kamati ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake Wilaya ya Kilwa kwa Kipindi cha Mwezi Januari mpaka Machi 2025, Kilichofanyika Mei 06, 2025 katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa Masoko.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Ndg. Hemed S. Magaro, amehimiza jamii kushirikiana kikamilifu na wadau wa maendeleo katika kuondoa kabisa vitendo vya ukatili na kushirikiana katika kuhakikisha upatikanaji wa Nyumba Salama na Kutambua Fitperson (Familia za Kuaminika) kwa ajili ya kuwatunza Manusura wa Vitendo vya Ukatili katika Jamii zetu.
Kilwa bila Ukatili wa Kijinsia inawezekana!
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa