Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imesaini makataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya Somanga na upanuzi wa hospitali ya Wilaya Kinyonga kwa bilioni 1.2
Mkataba huo wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia mbili (1.2bilion) umesainiwa katika viongozi wa wa Wilaya ya Kilwa na kampuni ya Pan African Energy ambao ni wadau wa maendeleo katika Wilaya ya Kilwa. Utiaji saini huo umeshuhudiwa na wawakilishi wa kampuni ya Pan African na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa. Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Ndg. Renatus Mchau ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo uliokuja kwa wakati na kueleza kuwa kwa muda mrefu Wilaya ya kilwa ilikuwa na changamoto katika sekta ya Afya lakini kwa sasa changamoto hizo zinakaribia kwisha kutokana na Halmshauri yake kuweka nguvu katika kuzitatu. ‘ Tangu mwaka 2017 tumepokea zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia nane kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI katika mpango wa uboreshaji wa sekta ya Afya ambapo vituo vine vya Afya vya Masoko, Tingi, Pande na Nanjilinji, na sasa mchango wa hawa wadau wametuongezea nguvu nyingine katika kuendeleza sekta ya Afya. Alisema msaada huo wa Pan African utaongeza idadi ya vituo vya Afya kutoka vitano vya sasa hadi sita ambapo kati ya hivyo vituo vine vitakuwa na uwezo wa kufanya upasuaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe.Abuu Mjaka amewashukru kwa mara nyingine kampuni hiyo kwa msaada huo kwani ni mara ya pili wanatoa msaada mkubwa baada ya ujenzi wa awali wa kituo cha Afya cha Nangurukuru. ‘Nyie sasa tunawatambua rasmi si kama wadau tu bali familia ya Kilwa’’ aliongeza Mhe.Mjaka. Kampuni ya Pan African wanashugulika na uchimbaji wa gesi katika kisiwa cha Songosongo kilichopo katika Wilaya Kilwa.
Ujenzi Kituo cha Afya cha Somanga ulianza kwa nguvu za wananchi ambapo mpaka sasa jengo la mapokezi lipo katika hatua ya linta kutokana na mchango wa wananchi , halmashauri pamoja mchango binafsi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dr.John Pombe Magufuli ya milioni ishiririni(20,000,000) aliyoitoa mwaka 2017 akiwa katika ziara mkoani Lindi. Mhe.Rais alitoa msaada huo baada ya kuombwa na wananchi waliomsimamisha katika kata ya Somanga, msaada huo ulikuwa chachu kwa wanachi wa kata hiyo na hivyo wakaanda kuchangia nguo zao.
Upanuzi huo utahusisha ujenzi wa Jengo la mapokezi,Jengo la wazazi, Upasuaji , chumba cha kuhifadhia maiti, Maabara na chumba cha kufulia nguo vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya milioni mia nane na thelathini ,Huku ktika hospitali ya Wilaya ya Kinyonga upanuzi utahusisha chumba cha kuhifadhia maiti na duka la dawa kwa gharama ya shilingi milioni mia nne.
Baada ya kukamilika kwa ujenzi Kituo cha Afya cha Somanga, Wilaya ya Kilwa itakuwa na vituo vya Afya sita ambavyo ni Somanga, Tingi, Masoko,Nanjilinji , Pande na Njinjo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa