Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (Kilwa DC) wameibuka washindi wa kwanza katika mashindano ya kitaifa ya uchoraji yaliyofanyika chini ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) mkoani Tanga, kuanzia tarehe 15 Agosti 2025 na kuhitimishwa tarehe 29 Agosti 2025.
Ushindi huo umetwaliwa na Jordanius Katunzi, Afisa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, ambaye aliibuka kinara katika mashindano hayo ya kitaifa ya uchoraji.
Mafanikio haya yameiweka Halmashauri ya Kilwa katika ramani ya kitaifa, yakionyesha kuwa pamoja na majukumu ya kiutendaji ya kila siku, watumishi wa serikali za mitaa wana uwezo wa kushiriki kikamilifu katika michezo na sanaa, na kuleta matokeo yenye heshima kwa taasisi na jamii kwa ujumla.
Aidha, ushindi huu unatarajiwa kuwa chachu ya kuimarisha mshikamano, ushindani chanya na mshikikano wa kijamii miongoni mwa watumishi wa umma nchini.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa