Kilwa.KUFUATIA uhamasishaji unaoendelea kufanywa na idara ya afya kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, kaya 10113 zimejiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) wilayani humu.Hayo ymeibainishwa jana kijijini Mtende, kata ya Kibata, tarafa ya Kipatimu na mratibu wa CHF wilaya ya Kilwa, Fred Mpondachuma alipozungumza na wananchi wa kijiji hicho katika uhamasishaji wa kujiunga na mfuko huo wa matibabu.Mpondachuma alibainisha kwamba idadi hiyo ya kaya zilizofikiwa zimesababisha kufikiwa wanufaika (watu) 62,000 waishio wilayani humu.Huku akiweka wazi kwamba zoezi la uhamasishaji unaoendelea umelenga kufikia vijiji 15 kati ya 90 vilivyopo wilayani humu kwa awamu hii.
"Lengo letu nikupata kaya 1000 kila wiki, jana na juzi pekee kaya 112 zilijiunga. ambapo Nanjirinji pekee zilijiunga kaya 56,"alisema Mpondachuma. Aidha Mpondachuma alitoa wito kwa watumishi wa idara ya afya wanaopangiwa kwenda kufanya kazi kwenye zahanati na vituo vya afya vilivyo mbali na miji na barabara kuu waridhike kwenda nakufanya kazi kwa moyo.Kwani mikataba ya ajira zao zinawataka wakafanye kazi popote ndani ya nchi hii. Mbali na hayo aliwaondoa hofu wananchi wilayani humo kuhusu huduma za afya zinazotolewa katika zahanati,vituo vya afya na hospitali kwani serikali imeboresha huduma hizo ikiwamo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba. Aliwaasa wananchi kutumia masanduku ya maoni yaliyopo kwenye maeneo ya kutolea huduma za afya kueleza kero na utoaji huduma za matibau zinazotolewa katika maeneo hayo.Kwani kamati zilizopo kwenye vituo vya afya na zahanati zinaundwa na wananchi wenyewe.Kwasababu kati ya wajumbe nane,mtumishi wa idara ya afya ni mmoja tu. Mratibu huyo aliwakumbusha na kuwahimiza wananchi kutunza na kulinda miundombinu ya zahanati,vituo vya afya ili iweze kuduma.Kwani fedha zinazotumika kufanyia ukarabati wa mara kwa mara zitaweza kutumika kununulia vifaa tiba na dawa. Kwaupande wake mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai licha ya kuwaasa wananchi kujiunga na mfuko huo. aliishukuru serikali kwa kuwapelekea watumishi 104 wa sekta ya afya hali ambayo itapunguza upungufu wa watumishi kwenye zahanati na vituo vya afya. Ngubiagai pia ametoa wito kwa halmashauri ya wilaya hiyo kupitia idara yake ya afya ihakikishe watumishi hao wanagawanywa kwa uwiano sawa ili kuondoa dhana kuwa watumishi wengi wanabaki mijini.Hali ambayo inasababisha malalamiko na manung'uniko kutoka kwa wananchi ambao zahanati na vituo vyao vya afya vipo mbali na miji. Wiaya ya Kilwa nimiongoni mwa wilaya za mkoa wa Lindi ambazo zimepokea fedha kwa ajili ya ukarabati wa vituo vyake vya afya.Kwamujibu wa Ngubiagai hadi sasa wilaya hiyo imepokea takribani shilingi 1.8 bilioni.Kwaajili ya ukarabati wa vituo vya Tingi,Masoko,Nanjirinji na Pande
Credit - Muungwana Blog