Katibu Tawala(RAS) Mkoa wa Lindi Zuwena Omary amefanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa Wilayani Kilwa
Katika ziara hiyo ambapo RAS ameambatana na Katibu Tawala (DAS) wa wilaya ya Kilwa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo pamoja na baadhi ya wakuu wa idara wa Halmashauri wamekagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Jengo la Halmashauri(Lingaula) ujenzi wa Madarasa,Mabweni na Nyumba za kuishi waalimu katika shule za Sekondari Mavuji,Somanga,Namatungutungu,Kilwa,Ilulu na Ngome
Zuwena amefanya ziara hiyo kwa lengo la kutambua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika zoezi la ukamilishaji wa mradi huo pamoja na kutathmini thamani ya majengo kulingana na fedha iliyotolewa na Serikali
Pia Zuwena amesema kuwa miradi hiyo imeletwa kwa ajili ya kuwanufaisha Wananchi na si kwa manufaa ya Viongozi,Hivyo amewataka Watendaji wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia kwa ufasaha miradi hiyo.
Aidha, RAS amewataka Wakandarasi waliopewa tenda ya miradi hiyo kukamilisha kwa haraka iwezekanavyo kwani ucheleweshaji wa miradi hiyo ni dhulma kwa watumiaji hususaji Wanafunzi wanaotakiwa kutumia majengo hayo
Kwa kumalizia amewapongeza Wakandarasi pamoja na Viongozi kwa jitihada wanazozifanya katika kusimamia ujenzi wa miradi hiyo, Pia amewasihi kushirikiana na Wananchi katika hatua zote za ujenzi kuwa miradi hiyo imetolewa na Rais kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wake.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa