Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imeandaa mpango wa kuanzisha vitalu vya malisho ya mifugo kwa vijiji ambavyo vimeanisha maeneo ya malisho ya mifugo katika mpango wa matumizi bora ya ardhi, Ili kuzuia mogogoro baina ya wakulima na wafugaji.
Hayo yamezungumzwa wakati wa Kikao cha Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa Tarehe 20/01/2025. Lengo la kikao hicho ni kujadili na kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Idara na Vitengo kwa kipindi cha Robo ya Pili ya mwaka wa Fedha 2024/2025.
Aidha Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hassan Swalehe (Diwani wa Kata ya Songosongo) amesisitiza ushirikiano wa wadau wote katika kutekeleza miradi ya maendeleo, pia ametoa pongezi kwa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa kuendelea kusimamia vyema utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa