Kilwa, 15 Julai, 2025
Kamati ya Huduma za Mikopo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imefanya kikao maalum kujadili taarifa ya uhakiki wa vikundi vya kijamii vilivyoomba mikopo isiyo na riba kwa kipindi cha Aprili hadi Juni, 2025.
Mikopo hiyo hutolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Dirisha la pili la utoaji wa mikopo lilifunguliwa mwezi Aprili, 2024 kupitia Wezesha Portal, mfumo wa kidijitali unaorahisisha uwasilishaji wa maombi ya mikopo katika ngazi ya halmashauri.
Katika kikao hicho, Kamati ilipitia na kujiridhisha kuhusu utekelezaji wa zoezi la uhakiki wa vikundi kwa kutumia fomu maalum pamoja na ziara za ufuatiliaji kwenye maeneo ya vikundi ili kuona shughuli halisi wanazozifanya. Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa mikopo inawafikia walengwa sahihi na kuchangia maendeleo ya kiuchumi katika jamii.
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imeendelea kujizatiti katika kuwawezesha wananchi kupitia utoaji wa mikopo isiyo na riba, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa matakwa ya kisheria ya kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya vikundi maalum.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa