Kamati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa wilayani Kilwa
Kamati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa Ndg. Alhaji Mjarufu wamekagua mradi wautoaji wa huduma za afya katika zahanati ya Tilawandu iliyopo kata ya Miteja wilayani humo iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi toka mwaka 2012 ambapo baada ya hapo Ofisi ya Mkurugenzi Mtendeji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa ilitoa kiasi cha milioni 50 kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati hiyo.
Akisoma Taarifa ya utakelezaji wa mradi huo Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Happiness Kapinga amesema kuwa wadau mbalimbali wa maendeleo wamefanya jitihada mbalimbali za ukamilishaji wa ujenzi wa mradi huo ambapo shirika la TCRS lilichangia shilingi milioni 3,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa, mfuko wa jimbo walichangia kiasi cha shilingi 2,000,000 pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi ilitoa milioni 50,000,000 hivyo na kuufanya mradi huo ukamilike na kuanza kutumika Disemba 2023.
Aidha kwa upande wake, mwenyekiti huyo wa CCM mkoa amewapongeza wananchi wa Kijiji hicho kwa jitihada walizozifanya za kujitolea katika ujenzi wa zahanati hiyo na kuwaahidi kuwa wao kama Chama hawatakuwa nyuma katika kuwashika mkono wananchi hao kwa ajili ya kuinua maendeleo katika jamii husika
Hata hivyo, ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani inatoa fedha nyingi katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za jamii katika maeneo yao ya karibu.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa