Tarehe 29/03 /2023 Kaimu Afisa lishe wilaya ya Kilwa DICKSON NG'UTO amewapongeza watumishi wa Zahanati ya Mandawa na kamati ya lishe ya kijiji kwa kuratibu maadhimisho ya siku ya afya na lishe ngazi ya kijiji ambapo wametoa elimu ya afya na lishe kwa jamii, wamepima hali ya lishe kwa watoto na watu wazima na kutoa elimu ya mapishi darasa ya chakula lishe.
Kwa kupitia hafla hiyo jamii ya kijiji cha Mandawa wamepata fursa ya kuudhulia na kushiriki na kutambua hali za lishe kwa ujumla na kupewa Elimu ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.
Ng'uto amefarijika kuona mwitikio mkubwa kwa wanajamii katika hafla hiyo kwani wameweza kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo na upimaji wa hali ya lishe kwa kupima watoto zaidi ya 80 na kati ya hao ni watoto 2 wamegundulika kuwa na utapia mlo wa kadiri.
Ametoa nasaha kwa wanajamii kuwa waendelee kuandaa na kushiriki vizuri katika maadhimisho ya siku ya afya na lishe.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa