Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Ndg. Zuwena Omary, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa kupata hati inayoridhisha kwa muda wa miaka 5 kuanzia mwaka 2019/20 hadi 2023/24 katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG).
Ndg. Zuwena ametoa pongezi hizo wakati wa Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) lililofanyika tarehe 19 Juni 2025 katika Ukumbi wa Sultani Kilwa Masoko.
Ndg. Zuwena amesema yote hayo yametokana na Halmashauri hiyo kuwa na ushirikiano, uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali zilizotengwa kwa ajili ya huduma kwa wananchi.
Hati hiyo inayoridhisha imetolewa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za mwaka 2023/24 ambapo Halmashauri ya Kilwa ilionyesha viwango vya kuridhisha vya usimamizi wa fedha na utekelezaji wa miradi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa