Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Ndg. Hemed Magaro amekabidhi jumla ya vishikwambi 53 vilivyotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa ajili ya wataalamu wa mifugo wa wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika tarehe 18 Septemba 2025 katika Ofisi za Halmashauri ya Kilwa, Ndg. Magaro amesema ugawaji wa vifaa hivyo ni hatua muhimu ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya sekta ya mifugo, hususan katika uratibu wa chanjo na utambuzi wa mifugo, ukusanyaji na utumaji wa taarifa pamoja na kuimarisha matumizi ya TEHAMA.
Kwa upande wake, Dr. Nyalekwa Mashimo, Mratibu wa Kampeni ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo Wilaya ya Kilwa, ametowa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa msaada huo. Amesema vifaa hivyo vitachochea maboresho ya huduma kwa wafugaji na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya wataalamu wa mifugo kuanzia ngazi ya kata hadi vijiji.
Aidha, Ndg. Magaro amesema mapokezi na mgao wa vifaa hivyo ni kielelezo cha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha huduma za mifugo, kuboresha takwimu pamoja na kusaidia kufanya maamuzi ya kisera na mipango ya maendeleo ya sekta ya mifugo nchini.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa