Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Abdallah Nyundo amezindua magari mawili mapya kati ya magari matatu yaliyonunuliwa ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa aina ya Toyota Hilux Double Cabin yenye namba za usajili SM 44152 na SM 44153. Magari hayo yamenunuliwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwa gharama ya Tsh. 447,583,373.55/=
Uzinduzi huo umefanyika tarehe 17 Septemba 2025 Katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Halmashauri hiyo kuboresha vitendea kazi na kuongeza kasi ya utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Nyundo amesema, ununuzi wa magari hayo ni kielelezo cha dhamira ya Serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, haraka na kwa ufanisi katika maeneo yote ya wilaya.
Magari hayo mapya yanatarajiwa kurahisisha usafiri wa watumishi kufika hata katika maeneo ya mbali yenye changamoto za kijiografia, jambo litakaloongeza ufanisi katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, utoaji wa huduma za kijamii, na ufuatiliaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Aidha, Halmashauri imepanga kuendelea kuongeza idadi ya vitendea kazi, ambapo katika mwaka wa fedha 2025/2026 imetenga shilingi 1,195,000,000 kwa ajili ya kununua magari matano zaidi; kati ya hayo, matatu kupitia mapato ya ndani na mawili kupitia ufadhili wa Serikali Kuu.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa