Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo ameongoza zoezi la ugawaji wa Vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo Ikiwa ni juhudi za kuwatambua wajasiriamali hao na kurahisisha shughuli zao za kibiashara, huku likilenga pia kuepusha changamoto za ulipaji wa kodi zisizo za lazima. Zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho limefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Zinga Kibaoni iliyoko Kata ya Zinga Miguruwe Tarehe 22/01/2025.
Akizungumza wakati wa kugawa vitambulisho hivyo, Mhe. Nyundo ameeleza kuwa vitambulisho hivyo ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo wanaozalisha chini ya shilingi milioni 4 kwa mwaka. Makundi wa Wajasiriamali hao yanahusisha makundi ya Machinga, Madereva wa Pikipiki na Bajaji na Mama na Baba Lishe. Pia ameeleza kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwezesha wajasiriamali hao kuendesha biashara zao bila usumbufu, na vitambulisho hivyo vinalipiwa shilingi 20,000 tu kwa miaka mitatu.
Hata hivyo, kati ya vitambulisho 102 vilivyolipiwa, tayari vitambulisho 78 vimegawiwa kwa wajasiriamali katika Kata za Miguruwe, Njinjo, Somanga, mingumbi Tingi, Manadawa na Kinjumbi hadi sasa. Mhe. Nyundo amewahimiza viongozi wa maeneo mbalimbali kuhimiza wajasiriamali wadogo wadogo kulipia na kuchukua vitambulisho hivyo ili kurahisisha uendeshaji wa biashara zao.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa