Ili kukuza uchumi utokanao na uvuvi wa kisasa nchini, serikali imetenga Juma ya Shilingi bilioni 266.7 kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya uvuvi katika Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi.Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mkataba na eneo la mradi kwa mkandarasi wa Mradi huo kutoka kampuni ya China Harbour Engineering Co.Ltd, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainab Telack amesema kwa mara ya kwanza serikali imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 100 ikiwa ni ya gharama za ujenzi wa Bandari Hiyo. Mkuu wa Mkoa amewataka wakazi wa kilwa kujiandaa kuupokea mradi ikiwa pamoja na kuwa tayari kupokea elimu itakayowasaidia kupata nafasi katika Bandari hiyo ya kisasa pindi utakapomalizika.Awali katibu mkuu wa wizara ya uvuvi na mifugo RASHID TAMATAMA amesema kuwa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka 2 ambapo kwa kuanzia serikali tayari imetenga bajeti ya shilingi bilioni 100Aidha,TAMATAMA amesema kuwa wanamini kwamba kama mkandarasi atatumia maarifa weledi na teknolojia ujenzi wa bandari hiyo itakamilika kwa wakati kulingana na makubaliano ya mkataba aliousaini Juni 7 2022.#Kazi iendelee
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa