Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa leo limefanya mkutano wa kujadili taarifa za utekelezaji wa kamati za kudumu za halmashauri kwa kipindi cha Robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025 (Januari hadi Machi 2025), pamoja na taarifa za utekelezaji wa kamati za maendeleo ya kata kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2025.
Mkutano huo umefanyika leo Tarehe 30/04/2025 katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (FDC) Kilwa.
Katika kikao hicho, madiwani wamepata nafasi ya kupitia na kujadili mafanikio, changamoto na mapendekezo kutoka kwa kamati hizo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuimarisha uwajibikaji katika ngazi zote za halmashauri.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Farida Kikoleka amewataka Viongozi na Wataalam kujikita katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unazingatia vipaumbele vya wananchi na kutekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyokubalika.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Hemed Magaro amewataka Wahe. Madiwani kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika kata zao ili kuweza kutatua changamoto za Wananchi wa Wilaya ya Kilwa.
"kukamilika kwa miradi yetu ni kuondoa Changamoto za wananchi kwahiyo tuendelee kusimamia kwa nguvu zote utekelezaji wa Miradi yetu" amesema Magaro.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa