Baraza la Biashara la Wilaya ya Kilwa limeendelea kujadili kwa kina mikakati ya kuimarisha sekta ya biashara na uwekezaji, huku likilenga kufuatilia na kubaini fursa mpya zitakazochochea ukuaji wa uchumi wilayani Kilwa.
Hayo yamejadiliwa katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika Tarehe 08 Oktoba 2025, chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Mohamed Nyundo, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa.
Miongoni mwa maeneo yaliyowekwa kipaumbele ni fursa zitakazotokana na bandari ya uvuvi inayojengwa wilayani Kilwa, ambazo zinatarajiwa kuongeza ajira, kukuza biashara, na kuongeza mapato ya wananchi pamoja na Serikali.
Kikao hicho pia kimejikita katika kujadili mwenendo wa shughuli za kiuchumi, changamoto zinazowakabili wafanyabiashara, pamoja na kuweka mikakati ya pamoja kati ya Serikali na sekta binafsi katika kukuza uchumi wa wilaya.
Aidha, wajumbe wamejadili hatua mbalimbali za kuhakikisha uwekezaji unaoendelea wilayani Kilwa, hususan katika miundombinu ya bandari ya uvuvi, unaleta matokeo chanya kwa wananchi. Pia wameweka mkazo katika kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha fursa hizo zinatumiwa ipasavyo kwa manufaa ya jamii.
Mhe. Nyundo amehimiza wajumbe wa baraza hilo kuendelea kushirikiana katika kuibua na kutumia fursa zote zinazojitokeza kwa maslahi mapana ya wananchi wa Kilwa. Aidha, amesisitiza kuwa ushirikiano wa dhati kati ya Serikali na sekta binafsi ni nguzo muhimu katika kufanikisha malengo ya kukuza uchumi wa wilaya.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa