Kilwa,
Wafugaji walioingia kinyemela na wanao miliki makundi makubwa ya mifugo katika kijiji cha Nakiu wametakiwa kuhamisha mifugo yao na kuipeleka sehemu zilkizotengwa kwa ajili ya mifugo.
Agizo hilo limetolewa jana juni 5 na mkuu wa wilaya ya kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai alipokua akizungumza na wakazi wa kijiji hicho katika viunga vya Ofisi ya Kijiji cha nakiu kufuatia malalamiko ya wakulima kuharibiwa mazao yao.
Ngubiagai amesema serikali imetenga maeneo kwa ajili ya wakulima na wafugaji makusudi ili kuondo migogoro ambayo imekua ikijitokeza mara kwa mara.
mkuu wa wilaya ya kilwa Mhe. Christopher Ngubiagaio kichukua maelezo kutoka kwa baadhi ya Wafugaji wanao sadikika kuwa na idadi kubwa ya Mifugo katika kijiji cha Nakiu (Picha: Ally Ruambo)
Pia amewataka wafugaji kufuga kwa kutumia njia za kisasa ikiwemo kufuga mifugo kulingana na ukubwa wa eneo ili kuweza kuwatunza vizuri.
“Ndugu zangu ardhi haiongezeki ila Mifugo inaongezeka, nani anaweza kuniambia toka azaliwe amewahi kuona ardhi ikiongezeka? kwahiyo tufuge kulingana na eneo tuliokuwa nalo ndio njia pekee kujiepusha na migogoro lakini kama eneo lako dogo na una mifugo mingi lazima itakushinda na kwenda kuharibu mazao ya watu.
Na mimi sitakuwa na msamaha kwa yeyote ambaye itathibitika kuwa mifugo yake imeingia na kufanya uharibifu katika shamba la mtu, kwa kua maeneo kwa ajili ya mifugo yapo na mimi siamini kama shamba linaweza kumfuata ng’ombe ila ng’ombe ndiye anayelifuata shamba” alisistiza Ngubiagai
Aidha Mhe. Ngubiagai amemuagiza Mkuu wa polisi Wilaya ya Kilwa kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wafugaji wote ambao wamekaidi amri halali ya kuhamisha mifugo yao kutoka kijiji cha Nakiu na kuipeleka katika maeneo yaliyopangwa kwa ajili mifugo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: +255 23 201 3241/65
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa