Kilwa,
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya kilwa imeridhia maombi ya Kampuni ya AMER-TAN INTERNATIONAL OF LOUSIANA ya kuwekeza katika wilayani Kilwa kupitia kilimo cha mpunga.
Maridhiano hayo yamefikiwa leo januari 6 mwaka 2018 katika ukumbi wa jumba la maendeleo baada ya kikao maalumu cha baraza la madiwani kilicho kaa kujadili maombi ya muwekezaji huyo aliyeomba kuwekeza katika kilimo cha mpunga.
Akizungumza na madiwani na Hadhira iliojitokeza katika kikao hiko mmoja wa wakurugenzi wa Amer-tan international of lousiana Bi. Halima Mamuya amesema Amer-tan imepanga kutumia Hekta Elfu kumi ambazo watazishughulikia katika awamu tofauti ambapo kwa kuanza wataanza na Hekta Elfu tano ambazo wanatarajia kuzalisha mpunga kiasi cha tani laki moja kila mwaka.
Amesema mpunga ambao utapatikana utaongezwa thamani kwa kuchakatwa kupitia kiwanda ambacho kitajengwa wilayani hapo.
Madiwani na wakuu wa idara mbalimbali wakiwa katika mkutano maalumu wa baraza la madiwani uliofanyika januari 6 katika ukumbi wa jumba la maendeleo wialayani kilwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kilwa Mh. Cristopher Ngubiagai amewashukuru waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya kilwa kwa umoja wao na kuridhia muwekezaji huyo kuwekeza katika wilaya ya kilwa na kuwaomba kujiweka mbali na mambo ambayo yatapelekea ugumu kwa wawekezaji ambao wanajitokeza kuwekeza wilayani kilwa ikiwemo kuwaomba kugharamia gharama za vikao.
Aidha Ngubiagai ameagiza wafugaji wote ambao wameingiza mifugo ya wilayani kilwa kinyume na utaratibu waondoke mara moja kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa juu yao.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: +255 23 201 3241/65
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa