• Malalamiko |
    • Anuani Zetu |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Kilwa District Council
Kilwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Mikakati ya Halmashauri
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Utumishi na Utawala
      • Elimu ya Msingi
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Maliasili
    • Vitengo
      • Usafi na Mazingira
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Biashara
      • TASAF
      • Lishe
      • Uvuvi
    • Miji Midogo
      • Masoko
      • Kivinje
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za Uwekezaji
    • Biashara na Viwanda
    • Madini
    • Uvuvi
    • Utalii
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Mikopo kina Mama na Vijana
    • Huduma za Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayo tekelezwa
  • Machapisho
    • Muongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Mifumo
    • PlanRep
    • FFARS
    • Prem
    • Salary Slip Portal

Elimu sekondari





Ndg.M.R.Mumini (DSEO)

HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA

TAARIFA YA IDARA ZA ELIMU MSINGI NA SEKONDARI KILWA FEBRUARI 2017

UTANGULIZI

Idara za Elimu Mingi na Sekondari zinajishughulisha na majukumu ya   Kusimamia, Kuinua na Kuboresha Maendeleo ya Elimu Wilayani. Aidha huduma zinazotolewa ni: Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Ufundi Stadi, Elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu, Elimu ya sekondari,  Elimu ya Watu Wazimu ambayo  imagawanyika katika sehemu kuu nne nazo ni Elimu Nje ya Mfumo, Elimu ya Ufundi,  Mukeja na MEMKWA.

Wilaya ina jumla ya shule za Msingi zilizosajiliwa 108 na shule za vitongoji (Satelite) 5 zenye jumla ya wanafunzi 52,127 kati yao wavulana ni 25,976 na wasichana  26,151.

UONGOZI

Idara  ya  elimu  ina  wakuu  wawili. Ambao ni  afisa  elimu  sekondari  ndugu  Mwinjuma Rajabu Mumini na  afisa  elimu  msingi Ndugu  Amosi  Kabula. Viongozi wengine  katika  idara  hizo  ni afisa  taaluma  sekondari ndugu Ernestina Mduma,  Afisa  takwimu  sekondari  ndugu Khajui  Bofu. Viongozi  wengine  wa  idara  ya  elimu  msingi  ni  Mafisa  taaluma  ndugu  Musa  Shabani  na  Yahaya  Mdidima, maafisa  takwimu  na  vielelezo  ni  Rehema  Mkalola  na  Mshamu  Ndandavale, Afisa  elimu  ya  watu  wazima  ni  ndugu  Salumu  Nampoto.  Afisa  elimu  maalumu  ndugu Mwanahiba  Mwichande, Afisa  Elimu  kilimo  ndugu  Omari  Mtimali, afisa  utamaduni  ndugu  Emanuel Paul, afisa  elimu  sayansi  kimu  ndugu  Rostabella  Lilali,  Afisa  Elimu  ufundi  ndugu  mshamu  mkundi,

Afisa vielelezo ndugu  mshamu  kiwanda  na  ndugu  Nafu apotei  ambaye  ni katibu  mhutasi

Kwa upande wa Sekondari Wilaya ya Kilwa ina jumla ya  Shule za Sekondari  27.  Kati ya hizo shule 26 ni za Serikali na  01  inamilikiwa na taasisi ya Dini ya Kiislamu, shule za Sekondari zina jumla ya wanafunzi 5,906 ikiwa wavulana 2,763 na wasichana 3,143. Shule za serikali zina jumla ya wanafunzi 5,696 na Binafsi 210.

Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Idara ya Elimu Msingi ina mahitaji ya walimu 1,295 waliopo ni 787 na upungufu ni 508.

Idara ya Elimu Sekondari ina mahitaji ya walimu 408, walimu waliopo ni 294 na ina upungufu wa walimu 114 kati yao 98 ni walimu wa masomo ya sayansi na Hisabati.

3.0IDARA YA ELIMU MSINGI

2.1 UANDIKISHAJI

Wilaya inaendelea Kuandikisha wanafunzi wa darasa la Awali na Darasa la Kwanza kama ifuatavyo:-

AWALI

DARASA LA KWANZA

MAOTEO
UTEKELEZAJI
MAOTEO
UTEKELEZAJI

WV

WS

JML

WV

WS

JML

%

WV

WS

JML

WV

WS

JML

%

4,220

4,053

8,273

2,056

2,162

4,218

50.98

3,441

3,146

6,587

4,071

4,008

8,079

122.65

 

2,2 MIUNDOMBINU (Madarasa, nyumba na vyoo)

 

Aina ya Majengo

Mahitaji

Yaliyopo
Upungufu
Vyumba vya madarasa

1150

732

418

Nyumba za walimu

787

303

 484

Matundu ya vyoo                    

2354

673

1618

 

2.3 MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA DARASA LA NNE (SFNA) MIAKA MIWILI (2015- 2016)

 

Shule za Msingi 106 zilisajili watahiniwa waliofanya upimaji wa Kitaifa wa darasa la IV 2015, na mwaka 2016 shule 103 zilisajili watahiniwa wa upimaji wa Kitaifa, taarifa za wanafunzi walioanza darasa la kwanza, waliosajiliwa kufanya upimaji, waliofanya, wasiofanya, waliofaulu na waliofeli zimeoneshwa katika jedwali lifuatalo:-

MWAKA

WALIOANZA DARASA LA I 2012 & 2013

WALIOSAJILIWA

%

WALIOFANYA MTIHANI  

%

WASIOFANYA MTIHANI 

%

WALIOFAULU MTIHANI

%

WALIOFELI

%

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

 

WAV

WAS

JML

 

WAV

WAS

JML

 

WAV

WAS

JML

 

WAV

WAS

JML

 

2015

3298

3190

6458

2692

2775

5467

84.65

2306

2538

4844

88.6

385

237

622

11.4

1904

2047

3952

81.56

402

3190

6488

2692

2016

3413

3341

6754

2438

2561

4999

74

2261

2452

4713

94.2

177

109

286

5.7

1992

2170

4162

88.31

269

282

551

11.69

Hali ya ufaulu ni ya kuridhisha kwa kuwa ufauli umekuwa ukipanda mwaka hadi mwaka, mwaka 2015 ufaulu ulikuwa asilimia 81.56 na mwaka 2016 ufaulu ulikuwa asilimia 88.31, ufaulu  ulipanda kwa asilimia 6.75.


2.4:  MATOKEO YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE) MIAKA MIWILI (2015- 2016)

 

        Wilaya ya Kilwa ina jumla ya shule za Msingi 108,  shule 104 zilifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2015 na shule 103 ndizo zilizokuwa na wanafunzi waliofanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi kwa mwaka 2016, taarifa za wanafunzi walioanza darasa la kwanza, waliosajiliwa kufanya mtihani, waliofanya, wasiofanya, waliofaulu na waliofeli, zimeoneshwa katika majedwali yafuatayo:-

MWAKA

WALIOANDIKISHWA DRS LA  I

WALIOSAJILIWA

WALIODONDOKA

WALIOFANYA

WALIOFAULU

WALIOFELI

WASIOFANYA


WV

WS

JML

WV

WS

JML

WV

WS

JML

%

WV

WS

JML

WV

WS

JML

%

WV

WS

JML

%

WV

WS

JML

%



2015

3363

3134

6497

1782

2050

3822

1581

1094

2675

41

1631

1937

3568

997

1027

2024

56.7

634

910

1544

43.3

151

103

254

6.6


2016

3152

2898

6050

1771

1955

3726

1381

943

2324

38.4

1741

1927

3668

1122

1133

2255

61.5

619

794

1413

38.5

30

28

58

1.56


        Hali ya ufaulu ni ya kuridhisha kwa kuwa ufaulu umekuwa ukipanda mwaka hadi mwaka, mwaka 2015 ufaulu ulikuwa asilimia 56.7 na mwaka 2016 ufaulu ulikuwa asilimia 61.5, ufaulu  ulipanda kwa asilimia 4.8.

 

 

 

 

IDARA YA ELIMU SEKONDARI 

 

 3.1 UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2017

 

Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2017 ni 2334, wakiwemo wavulana 1111 na wasichana 1,223. Hadi kufikia tarehe 17/02/2017 jumla ya wanafunzi  2,089 wakiwemo wavulana 1008 na wasichana 1,081  wamesharipoti shuleni.  Hii ni sawa na asilimia 90 ya wanafunzi wote waliotakiwa kujiunga na kidato cha Kwanza. Idadi ya wanafunzi ambao hawajaripoti mpaka sasa ni 245, wavulana 103 na wasichana 142  sawa na asilimia 10.  Halmashauri bado inafanya ufuatiliaji wa wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni ili wote waweze kuripoti shuleni. Jedwali la kuonyesha uandikishaji limeambatanishwa katika taarifa hii.

 

3. 2 SHULE ZA KIDATO CHA TANO NA SITA

Kuanzia tarehe 11/07/2016 Halmashauri  ilitarajia kupokea wanafunzi wapatao 86 ambao ndio  walipangwa. (Kilwa sekondari wavulana 46 na Ilulu sekondari wasichana 40) wa kidato cha tano.  Wanafunzi wote hawa ni wa mchepuo wa HKL. Wanafunzi walioripoti ni kwa shule zte mbili walikuwa 61 na waliohama au kwenda shule binafsi ni 16, na waliohamia ni 2.  Hadi kufikia tarehe 17/02/2017 wanafunzi waliopo ni 48, ambapo  Shule ya Sekondari Kilwa wapo wanafunzi 24 na shule ya sekondari Ilulu wako wanafunzi  24.

 

3.3 MIUNDOMBINU NA SAMANI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI

Lengo kwa sasa ni kuimarisha shule zilizopo kwa kuongeza Madarasa, Maabara, Hosteli na Nyumba za walimu. Ili kukabiliana na tatizo la mimba pamoja na utoro kwa wanafunzi Halmashauri imeweza kujenga hosteli 36 katika Shule za Sekondari 16. Pamoja na uwepo wa hosteli hizo bado kuna tatizo la wanafunzi kutokaa katika majengo hayo kutokana na tatizo la ukosefu wa samani za vitanda na ukosefu wa chakula. Aidha, kuna tatizo la upungufu mkubwa wa nyumba za walimu katika shule za sekondari, na upungufu wa maabara  pamoja na matundu ya vyoo kwa ajili ya walimu na wanafunzi , kama inavyoonekana kwenye jedwali.

 Idadi ya Miundombinu Katika Shule za Sekondari

AINA YA MIUNDOMBINU

MAHITAJI

YALIYOPO

UPUNGUFU

Nyumba za walimu

294

82

212

Vyumba vya madarasa

198

185

13

Matundu ya vyoo vya wanafunzi

256

229

27

Matundu ya vyoo vya walimu

52

22

30

Maktaba

26

3

23

Maabara

78

19

59

Mabweni

58

36

22

Mabwalo

26

2

24

Jengo la utawala

26

4

22

viti

5842

4682

1160

Meza

5842

4682

1160

NB. Upungufu wa madarasa upo kwenye baadhi ya shule hasa zenye wanafunzi wengi na baadhi ya shule zina ziada ya vyumba vya madarasa.

3.4 UJENZI  WA  MIUNDOMBINU  YA  SHULE

Wilaya  inaendelea  na  ujenzi  wa  vyumba  13  vya  Madarasa,  utengenezaji  wa  viti  na  meza  1160  katika  shule  za  sekondari  Kilwa,  Kivinje,  Ali  mchumo,  Namayuni,  Mpunyule,  na  Kiranjeranje  kwa  gharama  ya shilingi  344,380,000  kupitia  mapato  ya  ndani  ya  Halmashauri.  Ujenzi  wa  madarasa  umefikia  hatua  ya  umaliziaji.  Utengenezaji  wa  viti  na  meza  1160  unaendelea  ni  mategemeo  yetu  kuwa  ujenzi  utakamilika  mwishoni  mwa  mwezi  machi  2017

3.4 UTOAJI WA CHAKULA

Katika Wilaya ya Kilwa shule zinazotoa chakula kwa wanafunzi ni shule ya sekondari ya wasichana Ilulu na shule ya sekondari ya Kilwa kwa wanafunzi wa kidato cha tano.

 

3.5 MATOKEO YA UPIMAJI WA KIDATO CHA PILI KWA MIAKA MIWILI (2015 – 2016)

Matokeo ya upimaji wa mitihani ya kidato cha pili (FTNA) kwa kipindi cha miaka miwili (2015-2016) katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa yameonesha kuongezeka kwa asilimia 6.5 Wanafunzi waliofanya mitihani mwaka 2015 walikuwa 1153,waliofaulu walikuwa 955 sawa na asilimia 83 na waliofeli walikuwa 198 sawa na asilimia 17. Kwa mwaka 2016 wanafunzi waliofanya mitihani walikuwa 1200, waliofaulu ni 1074 sawa na asilimia 89.5,na waliofeli ni 126 sawa na asilimia 10.5

Jedwali la ufaulu mwaka 2015 na 2016.

Mwaka

Jumla ya waliofanya

Daraja

Waliofeli

% ya waliofaulu



I

II

III

IV



2015

1153

28

98

188

641

198

83

2016

1200

68
128
205
673

126

89.5

Majedwali yafuatayo yanaonesha ufaulu  kwa kila shule

3.6 MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KWA MIAKA MIWILI ( 2015 – 2016)

Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2015 na mwaka 2016 hayakuwa mazuri sana   kama inavyoonekana kwenye jedwali la matokeo kwa miaka husika.

Mwaka
Jumla ya watahiniwa

Daraja

Jumla ya Waliofaulu
% ya ufaulu
Waliofeli
% ya waliofeli
I
II
III
IV
 



2015
1110
2
32
88
460
582
52.17
528
47.83
2016
1043
1
46
116
426
589
56.0
454
43.2











Hali ya ufaulu kwa kidato cha nne  kwa miaka hiyo miwili inaonesha kuongezeka kwa asilimia 4 ijapokuwa  bado asilimia ya ufaulu iko chini. Nafasi ya wilaya kitaifa kwa mwaka 2015 imekuwa ya 164 kati ya 178, na kwa mwaka 2016 Wilaya yetu imeshika  nafasi ya 158 kati ya 178. Majedwali ya kuonesha ufaulu wa wanafunzi kwa miaka hiyo miwili yameambatanishwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

  4.0 MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA ELIMU

  • Halmashauri imeanzisha kidato cha tano kwa shule mbili za Sekondari ambazo ni Shule ya Sekondari ya wasichana Ilulu na shule ya Sekondari Kilwa kuanzia mwezi Julai, 2016.
  •   

Ongezeko la uandikishaji wanafunzi wa  kidato cha kwanza umeongezeka kutoka asilimia 72.1 mwaka 2016 na kuwa asilimia 90  kufikia mwezi wa Februari 2017.

 

Ongezeko la uandikishaji  wanafunzi wa darasa la kwanza umeongezeka toka asilimia  109.3  kwa mwaka 2016 na kufikia asilimia 122.65  kwa mwezi Februari, 2017.

Ongezeko la ufaulu kwa matokeo ya upimaji wa kitaifa  wa darasa la nne kutoka asilimia 81.56 mwaka 2015 hadi asilimia 88.31mwaka 2016, darasa la saba ufaulu ulipanda kutoka asilimia 56.7 mwaka 2015 hadi asilimia 61.5 mwaka 2016,  kidato cha pili ufaulu wa upimaji uliongezeka kutoka asilimia 83 mwaka 2015 hadi asilimia 89.5 mwaka 2016 na kidato cha nne ufaulu uliongezeka kutoka asilimia 52.17 mwaka 2015 hadi 56 mwaka 2016.

  • vii.    Kuanzisha vituo  5  vya MEMKWA kati ya vituo 10 vinavyotakiwa kuwapo.

 

5.0 CHANGAMOTO ZA IDARA YA ELIMU

  • Shule  za Msingi na sekondari  kushindwa kutoa  chakula cha mchana kwa wanafunzi, hii husababisha  utoro wa wanafunzi hivyo kupelekea  matokeo mabaya ya mitihani.

Shule kutokaguliwa na kutembelewa mara kwa mara.

  • Utoro wa wanafunzi na mimba kwa baadhi ya wasichana.
  • Upungufu wa miundombinu (madarasa, nyumba za walimu, maabara na vyoo) pamoja na samani kwa baadhi ya shule.
  • Upungufu wa walimu kwa shule za msingi na walimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwa shule ya sekondari

 

  • Jamii kutoshiriki ipasavyo  katika kuchangia maendeleo ya Elimu.
  • Wanafunzi kushindwa kujisomea baada ya kutoka shuleni.
  • Wanafunzi wa sekondari kushindwa kukaa shuleni hata kwas hule zenye hosteli

   6.0  MIKAKATI YA KUBORESHA ELIMU

  • Kuhamasisha wazazi na jamii katika kuchangia chakula cha wanafunzi shuleni
  • Kufanya ziara za ufuatiliaji mara kwa mara shuleni na kuwachukulia hatua  walimu na wanafunzi watoro
  • Kuanzisha klabu za wasichana ili kutoa elimu rika ambako kutasaidia kupunguza / kuondoa kabisa  mimba za wasichana
  • Kuendelea kutenga fedha kwenye bajeti kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, madarasa, vyoo na maabara.
  • Kuiomba Serikali iweze kutupatia walimu wa kutosha ili kukidhi upungufu uliopo.
  • Wazazi wawajibike katika kuwasimamia wanafunzi wao wapate muda wa ziada wa kujisomea

           Naomba kuwasilisha.

…………………..

ZABLON, I. BUGINGO

MKURUGENZI MTENDAJI (W)

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 04, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 11, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI. April 25, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DC KILWA AITAKA JAMII KUDHIBITI UTUMIAJI WA PLASTIKI ILI KUYALINDA MAZINGIRA.

    June 05, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAKIMBIZWA KILOMETA 173 NA KUTEMBELEA MIRADI 13 YENYE THAMANI YA TSH BILIONI 11 WILAYANI KILWA.

    May 31, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI ZAHANATI YA NJINJO KILWA.

    May 31, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI KWENYE MRADI WA UJENZI WA MNADA WA MIFUGO KILWA

    May 31, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Akipokea Mwenge wa Uhuru.
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • TARURA GPN
  • Watumishi Portal
  • MIKOPO 10%
  • Mikopo ya Wanawake na Vijana
  • Huduma za Elimu

Tovuti Muhimu

  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu
  • Lindi

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani Zetu

    Kilwa Masoko

    Anuani ya Posta: 160

    Simu: 0672365354

    Simu: 0672581557

    Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Kanuni Binafsi
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa